Kiungo Silva aaga Manchester City kimtindo

Wednesday June 26 2019

 

London, England. Kiungo David Silva amethibitisha hatokuwepo katika kikosi cha Manchester City (England) baada ya kuitumikia mara ya mwisho katika msimu ujao.

Kiungo huyo raia wa Uhispania ameweza kudumu kwa miaka 10 katika Ligi kuu ya Uingereza huku akichukua Ligi mara nne, Fa Cup mara mbili kombe la ligi mara nne.

“Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuwa hapa, miaka kumi inatosha sasa ni muda sahihi, klabu ilitaka kuniongezea miaka miwili lakini nazani muda sahihi sasa,” alisema.

Silva alisema amekuwa na wakati mzuri muda wote akiwa na klabu hiyo lakini anaona ni muda sahihi wa kurejea na kuwa karibu pamoja na familia yake.

“Nina familia hivi sasa na hili ndio jambo ninalolipa kipaumbele, nahitaji kutumia muda pia na familia, bado nina mwaka na Man City kwahiyo tutajua nini kitatokea baada ya msimu ujao,”.

Advertisement