Kisiga: Tukutane msimu ujao wa Ligi Kuu

Wednesday June 12 2019

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam.Kama ulikuwa unadhani kiungo Shaban Kisiga kafulia na kuishiwa kiwango, utakuwa umebugi sikia alichokizungumza bado yupo yupo sana katika Ligi Kuu ya TPL.

Kisiga alisema licha ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza na kurejea Ligi Kuu, haimanishi kwamba ameishiwa kiwango bali anaonyesha ujuzi wake popote anapopata nafasi.

"Soka kwangu ni rafiki, lipo kwenye damu kiasi kwamba siwezi kulifanyia kiki na ndio maana huwezi kukuta kiwango changu kinayumba popote nitakapocheza.

"Mazoezi na kuutunza mwili ni sehemu ya maisha yangu na ndio maana unaweza kukuta chipukizi wanavuna na kupotea, lakini sisi bado tunakuwa na hali ile ile.

"Msimu unaokuja nitacheza ligi kuu Bara, kuna timu ambayo namalizana nayo wiki ijayo, sisemi sana mashabiki ndio watakaoshuhudia kile ambacho nitakifanya, kikubwa ni kuomba uzima," alisema Kisiga.

Advertisement