Kisa Simba, Leopards: TFF yageuka mbogo

Monday September 10 2018

 

By Charles Abel

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa angalizo kwa klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata taratibu pindi zinapoandaa mechi za kirafiki na timu kutoka nje ya nchi.

Agizo hilo la TFF limekuja siku mbili baada ya Simba kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, Jumamosi jijini.

Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Salum Madadi alisema Simba iliitisha mechi hiyo bila kufuata utaratibu jambo ambalo limelishtua Shirikisho na kuamua kutoa angalizo mapema.

"Tumeamua kuwakumbusha hili kwa sababu hivi karibuni kuna timu mbili kutoka Kenya zilikuja nchini kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu za Simba na Biashara United.

Kwa bahati mbaya walioandaa mechi hizo hawakufuata taratibu za kikanuni za kuandaa mechi za kimataifa za kirafiki," alisema Madadi.

Advertisement