Kisa Diamond, msanii awajia juu mashabiki

Muktasari:

  • Hata hivyo kwa Diamond, Bahati kasema, sio kitu chepesi wao kuja kufanya kazi pamoja jinsi wanavyodhania mashabiki wake.

MWANAMUZIKI wa injili, Kelvin Bahati kawapa mashabiki wake jibu la kuchukiza ambao wamekuwa wakimshurutisha afanye kolabo na Diamond Platinumz.

Baada ya msanii Willy Paul, licha ya kuwa ni msanii wa injili, kuvunja mipaka na kufanya kazi na wasanii mbalimbali wasiokuwepo kwenye tasnia ya injili, mashabiki wa Bahati nao wamekuwa wakimsukuma ajaribu na hasa wakidai kolabo kati yake na Simba.

Hata hivyo kwa Diamond, Bahati kasema, sio kitu chepesi wao kuja kufanya kazi pamoja jinsi wanavyodhania mashabiki wake.

“Diamond ni mshikaji lakini pia kuna baadhi ya mashabiki wetu ambao hawafurahii tukijichanganya hivyo kwa misingi hiyo kidogo inakuwa ngumu. Halafu kama ikitokea tukashirikiana basi ni lazima wimbo huo wa kumsifu Mungu,” amesema Bahati.

Ifahamike kuwa tayari Bahati ameshafanya kazi na Rayvanny, Mbosso wote wa lebo ya Diamond WCB na vile vile Dogo Aslay