Kipigo cha Simba chawatibua Mbabane Swallows

Muktasari:

Simba ilianza kwa kuwasoma wapinzani wao,  huku ikilisogelea lango la Mbabane ambapo dakika ya  9, mkata umeme John Bocco alipenya safu ya ulinzi na kufyatua shuti lililofika mikononi mwa kipa.

Timu ya Simba imeibuka na ushindi mnono baada ya kuifunga  Mbabane Swallows mabao 4-0 ugenini, huku ikitinga hatua ya awali baada ya kuwa na jumla ya mabao 8-1.

Mabao ya mapema ya Simba yaliwafanya benchi la ufundi la Mbabane kufanya mabadiliko kw akumtoa beki Sifiso Mabila na kuingia Tarawallie Sallieu ambaye baada ya kutoka dimbani alianza kurumbana na benchi la ufundi kisha akasusa na kwenda vyumba vya kubadilishia nguo.

Simba ilianza kwa kuwasoma wapinzani wao,  huku ikilisogelea lango la Mbabane ambapo dakika ya  9, mkata umeme John Bocco alipenya safu ya ulinzi na kufyatua shuti lililofika mikononi mwa kipa.

Simba iliendeleza mashambulizi ambapo dakika ya 10 Emmanuel Okwi aliwakosakosa Mbabane, baada ya mabeki ha kujipanga vyema.

Dakika ya 19 Mbababe walifanya shambulizi ambapo mchezaji wao Hlatjwapo alikosa nafasi na mabeki wa Simba kuokoa shambulizi hilo.

Kiungo Cletus Chama alitumia vyema nafasi baada ya kumpangua beki wa Mbabane.

Kiungo huyo mshambuliaji hakufanya makosa katika dakika ya 33 ambapo aliwapangua kwa mara nyingine mabeki kasha kumpa pasi Okwi na Mganda huyo kumrudishia tena na kuwafanya wenyeji  kuzamishwa bao la pili.

Baada ya Simba kuonyesha kujiamini zaidi, Mbabane walijikuta wakifanya mabadiliko mengine dakika ya 39 baada ya kumtoa Richard Mccreesh na nafasi yake kuchukuliwa na Sikhondze ambapo licha ya mabadiliko hayo haikufanikiwa kuziona nyavu za Wekundu wa Msimbazi.

Hivyo dakika 45 za kipindi cha kwanza ilionekana Simba kuwa na nidhamu ya mchezo kutokana na kucheza kwa kujilinda huku wakifanya mashambulizi zaidi.