Kipigo cha Serena chasababisha Mjerumani kumwaga machozi

Muktasari:

  • Mjerumani huyo kwenye seti ya kwanza alijikuta akifumuliwa 6-0 na iliyofuata aliambulia 6-2 kwenye dimba la Rod Laver Arena.

Nyota wa tenisi duniani, Serena Williams amemshinda mpinzani wake Tatjana Maria kwenye mashindano ya Australian open, huku akiaga mashindano hayo kwa kumwaga machozi.

Serena ambaye ni bingwa wa mashindano hayo kwa mara ya saba, alitumia dakika 49 kumshinda mpinzani wake  ambaye seti ya kwanza hakuambulia kitu.

Mjerumani huyo kwenye seti ya kwanza alijikuta akifumuliwa 6-0 na iliyofuata aliambulia 6-2 kwenye dimba la Rod Laver Arena.

Ilimchukua dakika 19 tu Serema kupata pointi tano. Hata hivyo Maria alionekana kucheza kwa presha kubwa ili kuhakikisha anamshinda mpinzani wake.

Serena anasubiri mshindi wa mechi kati ya Eugenie Bouchard na Shuai Peng.

Kupigo kutoka kwa Serena kilionekana kumhuzunisha mwanadada Maria  licha ya mashabiki uwanjani hapo kumshangilia kwa upinzani alioonyesha.