Kipigo cha Man United shangwe kwa Man City

Sunday April 15 2018

 

London, England. Manchester City imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya Manchester United kufungwa bao 1-0 na West Brom.

Man City ilitwaa ubingwa huo baada ya bao la Jay Rodriguez katika dakika 73, na kuunyamazisha Uwanja wa  Old Trafford na kuwafanya kuwa nyuma kwa pointi 16 kwa vinara hao.

Man City ilipata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Tottenham kwenye Uwanja wa Wembley jana kuwaacha majirani zao katika presha kubwa katika mbio za ubingwa pamoja na kutibua sherehe katika mchezo baina yao uliofanyika Uwanja wa Etihad.

Man United walitakiwa wasipoteze mchezo wowote ili kuendelea na matumaini yao ya kupata ubingwa msimu huu, lakini mambo yalibadilika.