Kipchoge achana naye kabisa

Muktasari:

Dunia leo ilishangazwa na ukomo wa uwezo wa Bingwa wa Dunia wa Marathon na Olimpiki, Mkenya Kipchoge. Kumaliza mbio hizo kwa sekunde tisa mbele ya muda, uliishangaza Dunia na waandaaji wa INEOS 1:59 Challenge pia!

AMA kweli ‘No Human is Limited’. Ndio, kimombo ni kigumu lakini kutokana na alichofanya Eliud Kipchoge, kwa kukimbia mbio za kilomita 42, ndani ya muda wa saa 1:59:40, kimethibitisha kwamba, hakuna kinachoweza kumshinda Mwana wa Adamu akidhamiria.

Dunia leo ilishangazwa na ukomo wa uwezo wa Bingwa wa Dunia wa Marathon na Olimpiki, Mkenya Kipchoge. Kumaliza mbio hizo kwa sekunde tisa mbele ya muda, uliishangaza Dunia na waandaaji wa INEOS 1:59 Challenge pia!

Lakini amini usiamini, kama ulidhani ushindi huu umemshangaza Kipchoge basi unakosea sana. Kilichomshangaza Kipchoge pamoja wachache wanaofahamu uwezo wake, sio rekodi hiyo bali zawadi alizopewa.

Ni kwamba,  Kukimbia mbio hizo, kwanza kabisa kunamfanya Kipchoge mwenye umri wa miaka 35, kuwa mmiliki wa ndege binafsi aina ya Jet. Naam, Mfanyabiashara Bilionea JiMmy Wanjigi, ameahidi kumzawadi ndege hiyo kabla ya Novemba 28.

Ushindi huo, ambao ni wa kwanza kushuhudiwa, kunamfanya aingize mfukoni Ksh. Milioni 400  kutoka kwa wadhamini INEOS, Ksh 4.5 milioni kutoka kwa kampuni ya magari ya ISUZU na Ksh 10 milioni kutoka kampuni ya viatu ya NN na Nike.

Zawadi zingine ni Ksh 3 milioni kutoka Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Ksh 2 milioni kutoka Kaunti ya Nandi na nyingine 2.5 milioni kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, bila kusahau 15 milioni kutoka kampuni ya simu ya Safaricom na ubalozi wa bidhaa za kampuni hiyo.

Kipchoge, ambaye ni mshikilizi wa ubingwa wa Olimpiki, alitumia sekunde tisa mbele ya muda iliyowekwa na waandaaji wa mbio hizo za INEOS 1:59 Challenge, zilizomalizika muda mfupi uliopita Jijini Vienna, Austria