Kipa wa Arsenal atangaza kustaafu soka

Muktasari:

Kipa huyo mwenye miaka 36 alijiunga na Arsenal tangu Juni mwaka 2015 akitokea klabu pinzani ya Jiji la London, Chelsea ambako aliitumikia kwa miaka 11.

Kipa wa Arsenal ametangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio tangu mwaka  2015.

Kipa huyo mwenye miaka 36 alijiunga na Arsenal tangu Juni mwaka 2015 akitokea klabu pinzani ya Jiji la London, Chelsea ambako aliitumikia kwa miaka 11.

Alisema kucheza soka kwa miaka 15 kwenye Ligi Kuu ya England na kutwaa mataji  ni matumaini yake amefikia mafanikia aliyokuwa anayahitaji.

Alisema ataendelea kujituma ndani ya klabu yake huku akiwa na matarajio ya kutwaa taji msimu huu.

Cech alizua sinfahamu Oktoba mwaka 2006 baada ya kupata majeraha na kuhitajika kufanyiwa matibabu kutokana na kupasuka kutokana na kugongana na mchezaji wa Reading, Stephen Hunt.

Alilazimika kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu na tangu hapo akawa anavaa kifaa cha kujilinda sehemu ya kichwa.

Aliongeza kuwa huu ndio msimu wake wa 20 kwenye soka la kulipwa tangu aliposaini mkataba wake kwa mara ya kwanza ni miaka 20 sasa huku akisisitiza kwamba anaamini ni muda mwafaka kwake kutangaza kutundika daruga.