Kipa Yanga afiwa na baba yake

Muktasari:

Uongozi wa Yanga kupitia mtandao wa kijamii wa klabu hiyo wa Instagram umetoa pole kwa kipa huyo kutokana na msiba huo mzito.

Kipa wa Yanga,Klaus Kindoki amefiwa na baba yake mzazi  nyumbani kwao DRC Congo na mazishi yatafanyika Jumapili.
Uongozi wa Yanga kupitia mtandao wa kijamii wa klabu hiyo wa Instagram umetoa pole kwa kipa huyo kutokana na msiba huo mzito.
"Uongozi wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji Klaus Kindoki pamoja na familia yake kwa kumpoteza Baba yake. Msiba upo kwao Congo DRC na mazishi yatafanyika siku ya Jumapili huko huko kwao Congo" ilisomeka taarifa hiyo.
Kindoki yuko na timu mkoani Shinyanga wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage.