Kipa Simba yuko mbioni kutua Biashara United, Polisi

Muktasari:

  • Kipa, Emmanuel Mseja amemaliza mkataba wake na Simba na sasa anasaka timu ya kuichezea kwa msimu ujao

Dar es Salaam. Kipa wa Simba wa zamani, Emmanuel Mseja yuko mbioni kujiunga na kati Polisi Tanzania ua Biashara United katika kipindi cha msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mseja alishindwa kupata namba katika kikosi cha Simba msimu uliopita na kumlazimisha kujiweka pembeni akijifua binafsi.

"Naendelea na mazoezi, bado nasikilizia wapi nitakuwa kwa ajili ya msimu ujao ligi lakini kuna timu naendelea kufanya nao mazungumzo mambo yakiwa sawa nitakuwa huko zaidi ni Tanzania Prisons ua Biashara United," alisema Mseja.

Mseja anafanya mazoezi viwanja tofauti kama Gonga, Sinza na Gadren Kinondoni.