Kiki? Staa Hamilton amchana mpinzani

Muktasari:

Sasa baada ya Mercedes kuzindua gari lao litakalotumika ikiwamo na aina ya Mercedes W11, ni kama lililomfanya mpinzani wake Max Vestappen wa Red Bull kutokwa na maneno akisema endapo kampuni hiyo itampatia gari kama la Hamilton atamshinda bila kujali chochote kwa sababu yeye pia anamtegemea Mungu kushinda.

NI wivu tu! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na majibu aliyoyatoa dereva mkali kwenye mashindano ya magari kutokea kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton kwa mpinzani wake Max Verstappen wa Red Bull.

Iko hivi, timu mbalimbali zitakazoshindana kwenye mashindano ya Formula One mwaka huu yanazindua magari yao yatakayotumika kwenye mashindano ya Dunia ya Formula 1 ikiwemo Mercedes ya Hamilton.

Sasa baada ya Mercedes kuzindua gari lao litakalotumika ikiwamo na aina ya Mercedes W11, ni kama lililomfanya mpinzani wake Max Vestappen wa Red Bull kutokwa na maneno akisema endapo kampuni hiyo itampatia gari kama la Hamilton atamshinda bila kujali chochote kwa sababu yeye pia anamtegemea Mungu kushinda.

Hata hivyo, Hamilton akijibu kuhusu maneno yaliyotolewa na Vestappen, alisema kwake ni kama kituko tu na kwamba kila kitu anakifanya kwa vitendo kwenye mbio na sio kuhangaika na kinachosemwa vinginevo mhusika anathibitisha udhaifu wake.