Kichuya alianzisha, mtamkoma!

Muktasari:

African Lyon ni kama imemuibua upya Shiza Kichuya baada ya kuwafunga bao la kuongoza katika mechi waliocheza hivi karibu na Simba iliyowafunga mabao 2-1, kwani staa huyo ametamka moto wake hautapoa.

MASHABIKI wa Simba wamepigwa na ganzi baada ya kulishuhudia bao tamu la kideoni straika wao wa zamani anayekipiga Yanga kwa sasa, Ibrahim Ajibu, lakini winga wao Shiza Kichuya amewatuliza akidai ameliamsha na yajayo Msimbazi yanafurahisha.
Kichuya aliyetumia siku 222 (sawa na miezi saba na siku 10) ili kufunga bao lake la kwanza tangu alipofunga mara ya mwisho Februari 26, wakati Simba ikiiadhibu Mbao FC msimu uliopita kwa mabao 5-0, alisema bao dhidi ya African Lyon, limempa mzuka katika Ligi.
Winga huyo nyota alisema moto wake haupoi tena mpaka akaunti yake ya mabao inanona na kukiri alikuwa na wakati mgumu katika kipindi chote cha ukame wa mabao.
"Japo nilikuwa natotoa pasi za mabao, lakini nilikuwa natamani nifunge na Lyon imefungua njia ya kufanya makubwa zaidi, naamini nitatumia kuliko msimu uliopita."
Katika msimu huo, Kichuya alifunga mabao saba tu pungufu na misimu miwili aklipokuwa na mabao 12 akiwa kinara ndani ya Simba aliyokuwa akiicheza kwa msimu wa kwanza.
Kuhusu kuingia kwenye mbio za ufungaji bora, alisema ni vigumu kwa sasa kwa vile kuna ushindani mkubwa, huku akikiri kuwepo kwa mechi nyingi ni mtaji mzuri kwake.
"Mechi zinapokuwa nyingi ina maana mchezaji anapaswa kujituma ili kuwa fiti, mwili wake uweze kutumika muda mrefu, binafsi nimejipanga kadri siku zinavyokwenda."
Katika hatua nyingine nahodha wa Simba, John Bocco, amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kuonyesha kadi nyekundu kwa kumpiga beki wa Mwadui, Revocatus Mgunga.
Maamuzi ya kufungiwa kwa Bocco kulitangazwa jana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliyeeleza pia kupelekwa kwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa James Kotei wa Simba na Andrew Vincent 'Dante' wa Yanga kwa walifanya katika mechi ya watani.
Wambura alitangaza maamuzi mbalimbali yalifikishwa kwenye Kamati ya Saa 72 na hatua ambazo zimchukuliwa ikiwamo kesi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

 ndivyo ninavyotamani kuwa tofauti,"alisema.
Lakini kwa upande wa Ambokile ambaye anaongoza kufunga mabao sita hadi sasa alisema anajiona ana kazi nzito ya kuhakikisha anaendelea kuwa kinara dhidi ya wakongwe na wenye majina makubwa.
"Unajua kuna wachezaji ambao wanatajwa mbele ya wadau wa soka nchini hata mimi naona kama wana vitu adimu, kikubwa kwa sasa ni kuonyesha uwezo ndani ya dimba, bado ligi ni ngumu na ndefu hivyo nina kazi kubwa kuendelea kukaa kileleni,"alisema.

xxxxxxxx

Summary-African Lyon ni kama imemuibua upya Shiza Kichuya baada ya kuwafunga bao la kuongoza katika mechi waliocheza hivi karibu na Simba iliyowafunga mabao 2-1, kwani staa huyo ametamka moto wake hautapoa.