Kibadeni ataka wakongwe wasaidiwe

Muktasari:

Kibadeni aliyeichezea Simba kuanzia mwaka 1970 hadi 1978 ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Uwanja mpya wa Simba uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Amesema wakati wa ujana wao walitumia  nguvu zao kuitumikia Simba hivyo hawapaswi kusahaulika.

Licha ya kuwapongeza viongozi kwa kufanikiwa kutengeneza Uwanja wa klabu hiyo,Mchezaji wa zamani wa Simba Abdallah  King Kibadeni, amewataka viongozi hao  kuwasaidia wachezaji wa zamani na si kuwasahau.
Kibadeni aliyeichezea Simba kuanzia mwaka 1970 hadi 1978 ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Uwanja mpya wa Simba uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Amesema wakati wa ujana wao walitumia  nguvu zao kuitumikia Simba hivyo hawapaswi kusahaulika.
"Tuliitumikia Sana kwa ajili ya Simba,licha ya  ushawishi mwingi kutoka kwa wapinzani wetu lakini hatukwenda upande huo na tuliendelea kubaki Simba.
" Kuna wachezaji wengi waliitumikia Simba Ni wagonjwa mfano Shaaban Baraza na wengine, hivyo wasiachwe peke yao bali nao waangaliwe na wasaidiwe," amesema Kibadeni.
Wachezaji wengine wa zamani waliohudhuria uzinduzi huo ni Baraza na Malota Soma.