Khalid Chokoraa kupimana ubavu na Msaga Sumu leo Masai Club

Muktasari:

Lengo la shoo hiyo ni kuwapa burudani tofauti wakazi wa Kinondoni na maeneo ya jirani,kwani wakija  watapata muziki wa dansi na Singeli.

Mwanamuziki Khalidi Chokoraa,usiku wa leo anafanya shoo na bigwa wa Singeli Msaga Sumu katika Ukumbi wa Masai Club uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MCL Digital, Chokoraa amesema lengo la shoo hiyo ni kuwapa burudani tofauti wakazi wa Kinondoni na wamaeneo ya karibu,kwani wakija  watapata muziki wa dansi na Singeli.
Aidha Chokoraa amesema,shoo hiyo ni  ya pili katika kupiga  ukumbi huo tangu atoke  kambini Morogoro alipokuwa anaifua bendi yake ya Mapacha Watatu Original.
"Leo usiku patawaka Moto katika Ukumbi wa Masai Club,ukumbi ambao ni Mara ya pili kupiga toka nitoke kambini Morogoro muda wa miezi kumi,na niseme tu ni ukumbi ambao nitakuwa nafanya shoo kila Jumapili
" Na nimeona nitumie nafasi hii ya kufanya shoo leo na Msaga Sumu,lengo ni kuwapa radha tofauti wakazi wa Kinondoni na maeneo ya karibu,hivyo wakija watapata burudani ya muziki wa dansi na Muziki wa Singeli kwa shilingi Elfu tano tu  mlangoni."
Hata hivyo Chokoraa aliiambia MCL Digital kuwa,katika bendi yake amekuja na vitu vipya kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wategemee kuona wapiga vyombo wapya wenye ubunifu huku safu ya uimbaji ni wanamuziki wazoefu ambao ni Cathy Chuma,Fargason,Choki Junior  na Chokoraa mwenyewe.
Pia safu ya wacheza shoo sura mpya ambao ametoka nao Morogoro.