Kessy azawadiwa binti mrembo

Monday April 15 2019

 

By Eliya Solomon

KIWANGO cha beki wa zamani wa Yanga, Hassan Kessy, kimemkuna shabiki wa Nkana ya Zambia, Christopher Kadiwa ambaye ameibuka na kusema yupo tayari kumtoa binti yake kama zawadi kwa mchezaji huyo.

Kadiwa alisema kwenye mtandao wa kijamii kuwa anavutiwa mno na uwezo wa beki huyo ambaye licha ya kucheza nyuma anauwezo mzuri wa kushambulia kama winga.

“Wamepita mabeki wengi Nkana, lakini sijawahi kuona kama Kessy. Ni mjanja sana, anaweza kukaba vizuri na kushambulia.

“Siwezi kusita kumpa binti yangu tena siwezi kutaka hata mahari kwake. Ninachotaka kutoka kwake ni kumjali na kumthamini binti yangu tu,” alisema shabiki huyo.

Nje ya Bongo, ilimnasa Kadiwa ambaye anaonyesha wazi kumkubali Kessy kupitia mtandao rasmi wa kijamii wa klabu hiyo ambayo jana ilikuwa na mchezo mzito wa marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza ambao Nkana waliikaribisha CS Sfaxien ya Tunisia nchini Zambia waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Advertisement