Kessy aula Nkana apewa jezi namba 22

Muktasari:

Kessy aliyetupiwa virago na Yanga katika siku ya mwisho ya usajili wa Ligi Kuu Bara leo alionekana akiwa katika picha ya moja na viongozi na wachezaji wa Nkana FC iliyomsajili.

Dar es Salaam. ‘Ukisema cha nini mwenzako anasema atakipata lini’ ndivyo ilivyokuwa kwa beki wa Ramadhani Hassan ‘Kessy’ baada ya kutoswa na Yanga dakika za mwisho hatimaye amesajili wa Nkana FC ya Zambia.
Kessy aliyetupiwa virago na Yanga katika siku ya mwisho ya usajili wa Ligi Kuu Bara leo alionekana akiwa katika picha ya moja na viongozi na wachezaji wa Nkana FC iliyomsajili.
Beki huyo wa kushoto Kessy amepewa jezi namba 22, ikiwa ni ishara ya kuanza maisha mpya ndani ya Ligi Kuu ya Zambia msimu huu.
Uongozi wa Nkana FC, umemkabidhi Kessy  jezi namba 22, tofauti na aliyokuwa anaitumia Yanga namba 25, lakini pia Simba alikuwa anatumia  namna 4, wakati Mtibwa Sugar namba 2.
Kessy ameitumikia Yanga, msimu mmoja akitokea Simba, alionyesha kiwango cha hali ya juu, ambapo alikuwa panga pangua ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Mzambia George Lwandamina.