Kelly Haso kuachia wimbo mpya wa ‘Come Back'

Friday March 8 2019

 

Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa Band ya Bogoss,  Ally Saidi maarufu ‘Kelly Haso’ amesema wiki Ijayo Jumatatu anatarajia wimbo wake binafsi utakaoitwa Come Back.

Kelly Haso amesema wimbo huo utakuwa kwenye mahadhi ya Rhumba  na anaamini mashabiki watampokea kwa kuuunga mkono siku atakapouachia Jumatatu wiki Ijayo.

Akizungumza na MCL Digital, Kelly Haso alisema ameamua kufanya kazi hiyo akiwa na baraka kutoka kwa kiongozi wa kundi lake, Nyoshi El Sadaat.

Kabla ya kujiunga na Boggos, msanii huyo aliwahi kufanya wimbo wake unaofahamika kwa jina la Tunda ambao pia ulipokewa vyema na mashabiki wa muziki nchini.

Amesema kwenye wimbo huo mpya unaokuja, hajamshirikisha msanii mkubwa  ili aweze kujiimarisha zaidi.

Aliwaomba wapenzi wa muziki nchini kuupokea wimbo huo  huku akiahidi mambo mazuri zaidi yanakuja  kwani huo ni mwanzo tu wa ujio wake.

Advertisement