Kaze ampa mikoba Niyonzima

Muktasari:

Niyonzima hakuwa anapata nafasi kubwa ya kucheza chini ya kocha wa zamani Zlatko Krmpotic

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amempa jukumu zito kiungo wake Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa Ligi Kuu, Bara dhidi ya Polisi Tanzania unaoendelea katika Dimba la Uhuru Jijini.

Katika mchezo huo ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakukuwa na timu iliyoona lango la mwenzake, Niyonzima alionekana kucheza Jukumu la kiungo mshambuliaji.

Jukumu la Niyonzima ni kuamua muda gani timu ishambulie sambamba na kuhakikisha anakuwepo eneo lolote ambalo mpira utakuwapo bila kujali upo kwa timu pinzani ama upande wao.

Kwa zaidi ya asilimia 60, Niyonzima ameonekana kuyatimiza majukumu hayo ingawa amekumbana na changamoto kadhaa.

Changamoto mojawapo ni walinzi na viungo wa Polisi Tanzania ambao wameonekana kumkamia vilivyo kiungo huyo.

Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mukoko Tonombe.