Kavila anataka kuacha soka kwa heshima

Wednesday September 12 2018

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Akiwa anaelekea kutundika daruga kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavila amesema yupo makini kuhakikisha anafanya kitu kitakachoaacha kumbukumbu ndani ya kikosi hicho na Tanzania kwa ujumla.

Kavila alitangaza msimu huu kuwa wa mwisho kwake kucheza ligi kuu Bara, kwa kuwa umri wake umemtupa mkono na malengo yake atayaelekeza kusomea ukocha, ameweka wazi kwamba ana kazi malumu ya kufanya katika ligi inayoendelea.

"Katika mkataba niliousaini niliwaomba viongozi wangu wa Kagera Sugar, kwamba nahitaji uwe msimu wangu wa mwisho na ikitokea kozi ya ukocha waniruhusu kwenda kusoma, walikubali na baadhi ya mambo wanagharamikia wenyewe.

"Natamani historia ya kucheza kwangu miaka 10 msimu huu utakuwa mwaka wa 11 uwe na manufaa kwa wengine wanaokuja nyuma yangu ili wajifunze kutunza viwango vyao na pia kucheza kwa muda mrefu," alisema Kavila.

Advertisement