Katwila aibukia Ihefu

Sunday October 18 2020
katwila pic

KOCHA Zubery Katwila ameikacha Mtibwa Sugar na kuibukia Ihefu kuchukua nafasi ya Maka Mwalwisi aliyetimuliwa hivi karibuni licha ya kuipandisha Ligi Kuu Bara.

 

Ingawa mabosi wa timu zote wamekuwa wagumu kuanika ukweli wa jambo hili, lakini mtu wa karibu wa kocha huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa Katwila ameacha kazi ghafla Mtibwa baada ya kupata dili la Ihefu iliyowapotezea makocha Jackson Mayanja na Masoud Djuma waliokuwa wakizungumza nao.

 

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru alipoulizwa alisema hata yeye amesikia Katwila amejiunga na Ihefu ya Mbeya.

 

Advertisement

Kifaru alisema baada ya kutoka kufungwa na Gwambina walirudi na Katwila mpaka kambini, lakini juzi Jumamosi alipokea taarifa ya kuondoka kwa Katwila.

 

Kujua mengi kuhusu hatua hiyo ya Katwila, na uongozi wa Ihefu umesemaje soma gazeti la Mwanaspoti Oktoba 19, 2020

Advertisement