Katwila: Mtibwa ipo tayari kucheza na Simba muda wowote

Wednesday September 11 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam.Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kikosi chake kipokamili tayari kuivaa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katwila alisema hayo baada ya Bodi ya Ligi kurudisha nyuma mchezo wao dhidi ya Simba ambao ulipangwa kuchezwa Agosti 17 mwaka huu sasa utachezwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katwila alisema wamejiandaa kwa ajili ya timu zote kuhakikisha wanafanya vizuri hawana maandalizi spesho kwa Simba na timu nyingine hivyo wapo tayali kucheza na timu yoyote muda wowote.

"Tunawapa heshima wapinzani wetu kwa sababu ni mabingwa watetezi na wametoka kushiriki mashindano makubwa ya Ligi ya Mabingwa tutaingia kwa tahadhali lengo ni kuona tunapata matokeo," alisema na kuongeza kuwa.

"Wachezaji wangu wapo katika hari nzuri na wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza wa Ligi na tunakutana na timu ambayo imepata matokeo mazuri mchezo wao wa kwanza," alisema Katwila.

Advertisement