Katwila: Corona ni giza nene kwetu

Muktasari:

Amefafanua kauli yake kwamba licha ya kuwaambia wachezaji waendelee na programu za mazoezi, anaona haitoshi kurejea na kuwa kwenye ushindani wa juu kwa madai kuwa wachezaji nao ni binadamu hivyo watakuwa katika wakati mgumu wa kujilinda na maambukizi hayo.

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema hajapata picha namna Ligi Kuu Bara, itakavyomalizika msimu huu, kutokana na ugonjwa tishio wa corona.
Amefafanua kauli yake kwamba licha ya kuwaambia wachezaji waendelee na programu za mazoezi, anaona haitoshi kurejea na kuwa kwenye ushindani wa juu kwa madai kuwa wachezaji nao ni binadamu hivyo watakuwa katika wakati mgumu wa kujilinda na maambukizi hayo.
"Hatujui janga hili litaisha lini! Kwa sababu ni ugonjwa unaotulazimu tutulie nyumbani, hata ile kuwasisitiza wachezaji wakati mwingine inakosa nguvu maana mbele kuna giza nene hatujui lini tutakuwa huru,"
Ameongeza kuwa; "Nasubiri tangazo la serikali kama litaruhusu ligi iendelee ama kusogezwa mbele hapo ndio nitajua nifanyaje nini,"