Katiba ya Yanga yamuweka njiapanda Manji

Muktasari:

Furaha ya Wanayanga iliyopotea kwa siku 538 imerudi rasmi juzi Jumapili baada ya Baraza la Wadhamini la klabu hiyo kutangaza urejeo wa mwenyekiti wao, Yusuf Manji ambaye alijiuzulu wadhifa huo mwaka jana.

Tangu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji alipoandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti wa klabu hiyo, Mei 23 mwaka jana, mashabiki na wanachama wa Yanga waligomea uamuzi huo na kudai kuwa wanaendelea kumtambua kama mwenyekiti wao.

Soma hapa baadhi ya vifungu vya kwenye Katiba ya Yanga jinsi ambavyo vinaelezea nafasi ya viongozi klabuni hapo...

Katiba ya Yanga Ibara ya 28 kifungu cha (1) inasema Kamati ya Utendaji wa Yanga inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, wajumbe nane wa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu na wajumbe watano watakaoteuliwa na kamati tendaji, wawili kati yao watatoka Zanzibar.

Kifungu cha 3 kinasema mjumbe atakoma kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji iwapo atatenda au kufanya yafuatayo

(a) kujiuzuru kwa maandishi na kuwasirisha barua yake ya kujiuzuru kwenye kamati tendaji.

(b) hataudhuria mikutano minne mfululizo ya kawaida ya kamati kuu bila sababu za msingi

(c) Anashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo  kujiu

(d)Anapatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila mbadala wa faini.