Kashasha amchambua Bocco

Tuesday October 20 2020
KASHASHA PIC

MCHAMBUZI wa soka, Mwalimu Alex Kashasha amesema straika wa Simba, John Bocco ni jembe na ndiye straika hatari zaidi ndani ya kikosi hicho kwa mtazamo wake.

Kashasha ametamka kwamba kwake Bocco ni bora zaidi ya wenzake Chris Mugalu na Meddie Kagere. Amesema kwamba Bocco anauwezo wakutafuta mipira timu inapokuwa imenyang'anywa na akaweza kufunga akipita katikati ya mabeki.

"Ni kweli Kagere ni mtaalamu sana wa kufunga akisubiria mipira katika eneo lake, tofauti na Bocco ambaye muda mwingi anawapa presha mabeki kwa kuwapita akitoka na mpira mbali, kuhusu Mugalu nikipindi chake chakuonyesha ana nini kipya cha ziada kuliko hao wenzake,"alisema mchambuzi huyo ambaye kila Jumamosi ana kolamu maalum kwenye Mwanaspoti linalouzwa Sh500 tu.

Bocco ametupia bao moja tu kwenye Ligi Kuu msimu huu, amekosa mechi tatu mfululizo kutokana na majeruhi. Kagere ana mabao manne kwenye ligi huku Mugalu akiwa na matatu.

....

Advertisement