Kaseke aipa Yanga ubingwa msimu huu

Muktasari:

Kaseke anaamini msimu huu utakuwa wa mafanikio ya hali ya juu kwa Yanga, akiamini wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa  hivyo kubwa kwao ni kujituma bila kukata tamaa.

Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke amesema ataendelea kujituma ili kuacha alama ya kukumbukwa ndani ya klanu hiyo huku akimini  kuwa Yanga bingwa msimu huu.
Kaseke ambaye yupo kwenye kiwango cha juu kwa sasa akiwa ameshatoa pasi tatu za mabao kwenye Ligi Kuu Bara anaamini Yanga ndio itakuwa bingwa msimu huu baada ya watani wao Simba kuchukua mara mbili mfululizo.
Yanga imecheza mechi nane, imeshinda tano, imefungwa mmoja na sare mbili na  hilo wala halimpi presha Kaseke kwani naamini wakiongez bidii tu basi ubingwa unatua Jangwani msimu huu. 
"Kupoteza mechi moja na kutoka sare mbili hakuwezi kutunyama raha kwani bado kuna mechi nyingi mbele yetu, naamini Yanga tutachukua ubingwa,"
"Binafsi nafanya sana mazoezi ili niwe na mchango mkubwa kwenye timu yangu,natamani niache alama ya kukumbukwa kwamba niliisaidia kuchukua ubingwa kwa msimu huu,"amesema.
Mbali na kuamini kwamba Yanga wanaweza kuchukua ubingwa amekiri kwamba ligi ni ngumu inahitaji nidhamu ya juu ili kuweza kufikia malengo yao.
"Bila nidhamu ni ngumu  kuyatekeleza niliyosema,ushindani upo juu kila timu inahitaji matokea hivyo lazima tutoke jasho ili tuwe mabingwa,"amesema Kaseke