Kaseke: Usipojipanga inakula kwako

Muktasari:

"Naamanisha likizo ya lazima isimfanye mchezaji kujiona amepata nafuu ya kupumzika  bali ajichukulie kama ya kujenga kiwango kutokana na majukumu yaliyopo mbele yetu,"

WINGA wa Yanga, Deus Kaseke ameutazama msimu huu kama wa kutumika kikamilifu ili kuendana na hali halisi ya mpito wa ugonjwa wa corona.
Amefafanua kauli yake kwamba ligi endapo itaendelea wachezaji watatakiwa kuongeza nguvu zaidi kuliko walivyoanza awali.
"Naamanisha likizo ya lazima isimfanye mchezaji kujiona amepata nafuu ya kupumzika  bali ajichukulie kama ya kujenga kiwango kutokana na majukumu yaliyopo mbele yetu,"
"Kwa sababu ligi ikianza tutakuwa kama tunaanza moja, hivyo lazima kila mmoja wetu ajitathimini mwenyewe akiwa nyumbani na kuelewa mbele kuna kazi nzito zaidi ya tulipotoka,"amesema.
Amefichua namna anavyojifua kivyake akiongozwa na programu ya kocha wake kwamba inamsaidia kuutayarisha mwili wake kwa ajili ya kazi iliopo mbele yao.