Kapombe ashindwa kujizuia kwa mpwa wake

Muktasari:

Abas na Shomari ni ndugu waliokuwepo uwanjani kwa pamoja katika mchezo wa Simba dhidi ya Mwadui uliochezwa leo saa 10:00 jioni latika uwanja wa Uhuru.

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe ameshindwa kuficha hisia zake mbele ya mpwa wake Abasi Kapombe wa Mwadui baada ya mchezaji huyo kuumia katika mchezo huo.

Abas alishindwa kuendelea na mchezo dakika 77 na kutolewa huku nafasi yake akiingia Amri Msenda.

Baada ya mchezo kumalizika na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, Abas alibebwa katika machela na kupelekwa katika gari la wagonjwa lakini wakati mchezaji huyo anapelekwa Shomari alikuwa akihojiwa na alipoona ndugu yake anabebwa alimkimbilia..

Shomari alikimbia mpaka kwenye machela iliyombeba mpwa wake na kutaka kujua anaendeleaje kisha alivua jezi yake na kumpatia.

Inaelezwa kwamba Abas ameumia goti na amepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa ajili ya matibabu zaidi.