Kapama mchezaji bora Ndondo Cup

Saturday June 9 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya wa JKT Tanzania, Nassoro Kapama amechaguliwa mchezaji bora wa mchezo ufunguzi wa Ndondo Cup na kuondoka kitita cha Sh50, 000,  kutoka kwa wadhamini DCB Bank.


Kapama katika mashindano hayo anachezea Mabibo Market aliyoiongoza kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Keko Furniture katika mchezo wa ufunguzi.


Amechaguliwa kutokana na kuonyesha kiwanga cha juu katika mchezo huo na kupewa kitita hicho na wadhamini wao DCB bank.


Mchezaji huyo aliyeichezea Ndanda FC msimu ulioisha  alisema anashukuru kwa zawadi hiyo na kusisitiza kupambana katika mechi nyingine.

Advertisement