Kangwa aipotezea Azam

Saturday December 8 2018

 

By THOMAS NG’ITU

BEKI tegemeo katika kikosi cha Azam, Bruce Kangwa, anakaribia kumaliza mkataba klabuni hapo lakini ni kama amepotezea kuongeza mpya.
Kangwa amekuwa mchezaji tegemeo katika ukuta wa Azam akilinda zaidi upande wa kushoto na kupandisha mashambulizi, haonekani kuwa na mpango wa kusaini dili jipya.
Mwanaspoti linafahamu mkataba wa beki huyo unamalizika mwishoni mwa msimu na mabosi wa Azam wamekuwa na kawaida ya kuwaongezea mikataba nyota kabla hawajamaliza, lakini kwake imekuwa tofauti.
Hata hivyo, mwenyewe ameliambia Mwanaspoti kuwa kwa sasa bado hajaweka akilini mambo ya kufuatilia mkataba mpya.
“Akili yangu ni kutaka kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu, malengo ya timu yatimie halafu hayo mengine yatafuata tu,” alisema na kusisitiza kwamba: “Mwalimu ndio atajua kama nataendelea hapa au vipi, binafsi nina mipango yangu lakini kama natafuta kitu ambacho hata hapa basi nitakuwepo.” 

Advertisement