Kambi ya Neymar yateta na Man United

Tuesday February 12 2019

 

KAMBI ya staa wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar imeiambia Manchester United haijaondoa uwezekano wa staa huyo kutua Ligi Kuu England dirisha kubwa lijalo la majira ya joto.

Mpaka sasa inadaiwa Real Madrid wamerudi tena katika kinyang’anyiro cha kumchukua Neymar dirisha kubwa lijalo na wanaongoza katika mbio hizo huku Barcelona wakiwa bado hawajaonyesha nia ya dhati ya kumrudisha.

Kwa muda mrefu Man United wamekuwa wakihusishwa na staa huyo na wamekuwa na mawasiliano ya karibu na kambi yake na kuna uwezekano mkubwa wakaweka dau litakalovunja rekodi ya uhamisho wa dunia kama Neymar akikubali kutua Trafford.

Neymar alitua PSG akitokea Barcelona msimu wa 2017 baada ya kucheza kwa misimu mitatu ya mafanikio akifunga jumla ya mabao 69 kwenye mechi 123. PSG ameifungia mabao 32 katika mechi 33 alizocheza hai sasa.

Advertisement