Kambi ya Moro Yanga yamkuna kocha Zahera

Tuesday August 7 2018

 

By Khatimu Naheka

Morogoro. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kama kuna kitu uongozi wao umekifanya kwa akili ni kuandaa kambi ya Morogoro.
Zahera amesema kwa sasa anaiona timu yake ikiwa na mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake kuiva kama anavyotaka.
Kocha huyo amesema anawaona wachezaji wake wakiwa na mabadiliko makubwa kulinganisha na walivyocheza mechi mbili za hatua ya makundi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ambazo walipoteza nyumbani na ugenini.
Aidha Zahera amesema endapo timu yake ingekuwa na maandalizi waliyonayo sasa Yanga isingeweza kufungwa na Gor au hata kutoa sare.
"Nimefurahi sana kwa hii kambi, wachezaji wanakula vizuri na kupumzika ninavyotaka, ukiangalia wamekuwa na mabadiliko makubwa," amesema Zahera.
"Hiki kilichofanywa na uongozi kilipaswa kufanyika muda mrefu, kama tungepata maandalizi haya Gor Mahia wasingetufunga.

Advertisement