Kama vipi wana bora tu, mkaushie majani mapema

Friday November 9 2018

 

By MZEE WA KITAA

LONG taim wana tumekuwa tukiwatonya kimtindo, jamani jani halifai....jani baya lakini mkajifanya makauzu!
Kitambo tumekuwa tukiwa-alati, jamani jani baya...Majani si rafiki kwa ndinga lenu, lakini hakuna aliyetubilivu...kuna wana wengine walituona sisi wakuda tu...eti tunawakata stimu tu!
Sio siri kuna wana wengine wanapiga jani hadi jicho linakuwa nyanya...halafu wanakuwa kama roboti tu graundini...samtaim wanafanya vimbwanga na vibweka vya kishamba ile mbaya...!
Mnabisha nini? Si mnakumbuka ile njemba ya Wagonga nyundo enzi zile alivyojifanya konki..konki oili chafu... konki masta...na kumpima kepteni pale Mbande...ghafla tu akala mvua mbili fasta!
Halafu sasa ile anatoka lokapu tu, hata hajakaa sawa akampa mtu cha chembe, kama mgosi Mwakinyo... akala kibano tena!
Ila nini, tuelewane mapema...alichokifanya konki msela masta inaweza isiwe ishu ya  jani, lakini kwa akili za kawaida unaweza kufili, hivi mwana timam ambaye hajakutana na bobumale kweli anaweza kufanya uduwanzi kama ule? Lazima tu awe amevuruga netiweki kiaina kwa kutafuna au kupuliza!
Enewei...nilitaka kutonya tu, bila shaka kibano alichopewa Mudi wa pale Kifusini kutoka kwa wale jamaa zetu wa zoni faivu...bila shaka iwahelpu kuwaamsha wana kimtindo, wajue mapema kuwa, wakizubaa inaweza kula kwao...wanaweza kuamka wanidei bila kujua kama kuendekeza kwao jani ni noma, wanaweza wakajikuta wakiumbuka kama mshkaji wao Mudi!
Maana inaweza kutokea dei, hawana hili wala lile, ghafla wazee wakatimba graundini kama ilivyomshtukiza Mudi na washkaji zake wengine wa Hiroiz, kisha mkatakiwa kufanyiwa chekapu ya fastafasta....halafu sasa kumbe lasti naiti wana mmepuliza sana bobumale hadi maji mkaita mma dadaadeki!
Mzee wa Kitaa kwa eji yangu najua kuna wana kibao, bila hiyo midude netiweki zinafeli, bolu halipigwi kabisa na wanakuwa ovyo kinoma, yaani jani kwao ni kama stata ya kupiga mzigo...! Ni sawa na wale mayanki ambao bila mkashari na mkuyati ama supu ya pweza mambo hayaendi kabisa kwa vidamshi...ila  nini wana hiyo kitu ni noma kwa laifu ya ndinga lenu na hata laifu ya kawaida...Mudi kala mvua ya kishkaji tu, lakini kwa ishu yake angechezea mvua nyingi kama ya kina Mang'ana ama ya advoketi msomi aliyepigwa juzi kati na ile kamati ya Mzee Baba ambaye kila akiitisha presi basi jua kuna mwana anaenda lupango kwa long temu....! Eti kuna washkaji wananitonya Mzee Baba akikuita frontofu kizimbani anakuchana laivu bifoo...kaa hapo tukupe kibano...haahaa...kama ni kweli mdingi noma sana!
Kwa wanaokumbuka kipindi flani, Tifuatifua ya Mkandarasi wa kule Kiraracha, aliwahi kuibua ishu ya kutaka wana wapimwe kila sizoni, ili kujua wamelodi mzigo kiasi gani, yaani alkoholu..
Hata hivyo inadaiwa ishu ilidedi kimya kimya kwa vile malida wa zile klabu za kina sunche na kapeto hawakutaka kwa kuhofia kukosa majembe wa kuzipigia...! Inaelezwa huko ndiko jani na midude mingine ya hatari linatafunwa kinoma noma katika kempu zao, yaani wana wanakula jani kama hawana akili na hakuna wanaowakemea kwa vile hata baadhi ya malida nao ni memba wa hiyo ishu na vilevi vingine!
Ni kweli kila mwana na starehe yake, lakini jani a.k.a mineli kispoti ni noma...si jani, hata mapouda... sijui ulabu na midude mingine ya hatari...kwani ikitokea wana mkataitiwa mkapimwe, walahi mtaumbuka kuliko Mudi...Longtaim ago jani halikuwa ishu sana kispoti, lakini nao e dei limeungwa na midude...!
Hivyo jichanganyeni mje kuumbuliwa, ikiwezekana ikaushieni tu mapema ili muwe sefu...vinginevyo mtalia...ooh shauri yenu!

Advertisement