Kama hukushiriki Olimpiki, huku huna chako kabisa

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema, msimamo huo wa ANOCA umepitishwa katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Kamati za Olimpiki uliofanyika hivi karibuni nchini Malawi.

SIO siri tena, huu ndio ukweli na tayari ANOCA imepitisha msimamo kwamba hivi sasa hakuna mwanamichezo atakayeruhusiwa kugombea uongozi wa Kamisheni ya wachezaji kama hajashiriki michezo ya Olimpiki.

ANOCA au Chama cha Kamati za Olimpiki Afrika kimesisitiza, wagombea wa kamisheni hiyo sio tu wawe wameshiriki Olimpiki, ila pia wawe wameshiriki

Olimpiki tatu mfululizo kabla ya kugombea.

Msimamo huo wa ANOCA unawaweka njia panda wanamichezo wa Tanzania ambao nchi yao ilikuwa ikitoa nafasi kwa wanamichezo waliowahi kushiriki michezo ya Afrika (All Afrika games) na Michezo ya Madola kuongoza kamisheni hiyo ambayo inafanya uchaguzi kila baada ya miaka minne.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema, msimamo huo wa ANOCA umepitishwa katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Kamati za Olimpiki uliofanyika hivi karibuni nchini Malawi.

“Watakaoruhusiwa sasa kugombea kwenye uchaguzi wa Kamisheni ya 2020 ni wanamichezo walioshiriki Olimpiki kati ya 2012 nchini Uingereza, 2016 nchini

Brazil au ile ya 2020 nchini Japan, kinyume na hao hatoruhusiwa kugombea, wanamichezo wenye nafasi hiyo sasa ni wanariadha, Faustine Mussa, Zakia Mrisho, Fabiano Joseph, Said Makula, Sarah Ramadhan na Alphonce Simbu, mchezaji judo, Andrew Thomas, bondia Suleiman Kidunda na waogeleaji, Magdalena Mosha na Hilal Hilal.