Dreamliner yaota mbawa kusafirisha kikosi Stars

Tuesday October 9 2018

 

By THOMAS NG'ITU

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe, amefichua kwamba ndege ya serikali 'Dream Liner' haitosafirisha kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania, baada ya kupata changamoto ya uwanja watapotua Cape Verde.
Awali, ndege hiyo ndio ilikuwa ikipigwa chapuo lakini imebidi wabadilishe kutokana na changamoto ya uwanja wa kutua.
"Tumemtuma Mgohi aweze kuangalia namna sehemu ilivyo tutakayofikia, ametuambia kwamba uwanja ni mdogo kwahiyo tumeongea na wenzetu wa Airt Tanzania na tumeagiza ndege nyingine ambayo ina usajili wa Tanzania ambayo ina weza kushuka na kupaa kiurahisi," alisema.

Wakati huohuo kambini hapo walifika makipa wawili Benedict Tinocco (Mtibwa) na Aaron Kalambo (Prisons) hali ambayo inaweka hati hati ya makipa Beno Kakolanya aliyeshtua nyama za paja pamoja Abdulrahman Mohammed aliyepata majeraha ya enka.

Advertisement