Kahata: Mbao FC walikuwa na bahati

Friday January 25 2019

 

By OLIVER ALBERT

KIUNGO wa Gor Mahia, Francis Kahata amesema  bahati tu ndiyo iliwabeba Mbao FC katika mchezo wao wa robo fainali ya mashindano ya Sport Pesa.
Gor Mahia ambao walikuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo walitolewa hatua hiyo baada ya kufungwa na Mbao FC kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bapo 1-1.

Kahata ambaye aliingia kipindi cha pili katika mchezo huo alisema waliupiga mpira mwingi lakini bahati haikuwa yao.
“Tulicheza vizuri kuanzia kipindi cha kwanza hata cha pili. 
“Niseme wapinzani wetu(Mbao) walikuwa na bahati katika mchezo huo kwani kama tungeongeza nguvu kidogo na kuwa makini tusingefika kwenye matuta,” alisema Kahata.
Katika mchezo huo Gor Mahia ndio ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 52  lililofungwa kwa Penalti na Dennis Oliech kabla ya Mbao kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Raphael Siame. 
Walioifungia Gor Mahia ni Francis Kahata, Jacques Tuyisenge na Boniface Omond wakati Harun Shakavah na Shafik Batambuze walikosa.
Mbao ilifunga penalti zao kupitia kwa Said Khamis, Raphael
Siame, Hamimu Abdukarim na David Mwasa.

Advertisement