VIDEO: Kagere amuinua Mo, Chama apiga bao la kideo

Muktasari:

Goli alilofunga mshambuliaji Meddie Kagere lilinfanya bilionea Mo Dewji kusimama na kushangilia kwa shangwe

Dar es Salaam. STRAIKA Meddie Kagere wa Simba amemuinua mdhamini wa klabu yao Mo Dewji jana Jumatano baada ya kufunga bao la tatu katika mchezo huo.

Kagere aliweza kuwachomoka vizuri mabeki wa Mbabane Swallows na kufanikiwa kuweka mpira wavuni huku akimuacha kipa wa wapinzani wao akiduwaa.

Goli hilo lilimfanya tajiri huyo asimame kwa kuning'inia baada ya kumuona mchezaji huyo amekimbia mpaka usawa wake na kuonyesha nembo ya kubusu jezi ya timu hiyo.

Wakati huo huo mabadiliko ya Simba kwa kumtoa John Bocco na kuingia Hassan Dilunga, yalionyesha tija kwani kiungo huyo baada ya kuingia aliweza kupigiana pasi za haraka na Clatus Chama na kumfanya Chama afunge goli la nne.

Goli la Chama ni la kideo baada ya staili yake aliyotumia kufunga kwa kuweza kuwadeshi mabeki wa Mbabane na kisha kupiga shuti la chini lilimshindwa kipa wa Mbabane.

Uwepo wa Mohammed Dewji katika uwanja wa Taifa umeonekana kuongeza morali kwa wachezaji wa Simba.