Kagere,Okwi, Bocco waikosa Nyasa Big Bullet

Muktasari:

  • Simba itacheza na Nyasa Big Bulle kwenye mchezo wa kirafiki keshokutwa Ijumaa huku ikiwakosa nyota wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali.

Dar es salaam. Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet

Hata hivyo katika kuelekea katika mchezo huo, Manara alisema maandalizi yanakwenda vizuri, wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo isipokuwa nyota wao walioitwa katika timu zao za taifa.

Nyota watakaoukosa mchezo huo ni Aishi Manura, John Bocco, Shiza Kichuya, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na Chama.

Simba inacheza mchezo huo wa kirafiki huku ikiwa kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi Kuu ambayo imesimama kupisha mechi za kimataifa kufuzu Afcon 2019.