Kagera yaichomoa Simba kilele

Friday November 22 2019

 

By THOBIAS SEBASTIAN

USHINDI wa mabao 2-1 ambao wameupata Kagera Sugar dhidi Lipuli FC nyumbani umewapandisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi huku Simba ikishusha nafasi ya pili kwani wana pointi 22 hadi sasa.
Kagera wamefikisha pointi 23 wakiwa wamcheza mechi 11 mbele ya Simba ambayo imecheza mechi tisa na kesho Jumamosi wataikaribisha Ruvu Shooting uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika michezo hiyo ya Kagera, wameshinda mechi sita, wamepoteza mechi miwili wakisuluhu mechi mbili na kufunga mabao 16 na kufungwa mabao tisa.
Michezo mingine iliyochezwa leo Ijumaa, Namungo kwa mara ya kwanza msimu huu wakiwa nyumbani uwanja wa Majaliwa uliopo Luangwa Lindi, wamekubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Alliance nao wakiwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza wameifunga KMC mabao 2-1 huku Ndanda nao wakipoteza nyumbani Uwanja wa Nangwanda Sijaona dhidi ya Polisi Tanzania mabao 2-0.
 Tanzania Prison wenyewe wameendeleza ubishi wao wa kutokubali kufungwa msimu huu baada ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya Mwadui uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Advertisement