Kabanda: Ligi Ifutwe tu Tanzania

Muktasari:

Janga la corona limepelekea Ligi  nyingi Duniani kusimama  huku kukiwa kuna uwezekano wa baadhi ya nchi kufuza ligi zao kutokana  maambukizi ya ugonjwa huo kuzidi kushika kasi.

Beki wa Kushoto wa Namungo Fc, Jukumu Kibanda  amesema kama janga la virusi vya corona litaendelea na Ligi Kuu Bara ikafutwa, itakuwa safi kwani kila kitu kinatokea kwa sababu na hakuna kitu muhimu kama afya njema.
Mchezaji huyo amesema wanazidisha  maombi ili janga hilo limalizike na warejee uwanjani lakini kama itashindikana hawana budi kukubaliana na hali halisi.
"Sasa hivi nchi nyingi zinaumiza kichwa ni jinsi gani watamaliza ligi ikiwemo hapa nchini kwetu kutokana na jinsi maambukizi ya ugonjwa huu yanavyoshika kasi.
"Kama mimi natamani hali hii isiendelee na turudi kumalizia mechi za ligi na kila mtu avune alichopanda lakini kama hali itakuwa mbaya zaidi basi itabidi  msimu huu tusamehe tu kila kitu tulichofanya uwanjani na tuanze msimu mpya.
" Afya ni bora kuliko michezo hivyo endapo itatokea ligi ikasitishwa basi aliyekuwa anaongoza ligi na  wa pili watuwakilishe kinataifa.
" Pia zile timu zilizokua zinatakiwa kushuka zisishuke na tuanze msimu mpya na zile ambazo zilikuwa Ligi Daraja la Kwanza na zikawa katika nafasi nzuri ya kupanda inabidi zivumilie tu na kucheza tena msimu mwingine ili kutafuta nafasi kwani naamini kama  wana timu nzuri hawatapata tabu ya kufanya vizuri tena ingawa jambo hilo litakuwa linawaumiza lakini haina jinsi kwani hakuna aliyeomba huu ugonjwa utokee Duniani" amesema Kibanda.