KVZ, Jamhuri zatoshana nguvu dakika 45 za kwanza

Muktasari:

Jamhuri ilikuwa na nafasi nzuri ya kuongoza dakika 45 za kwanza lakini ikashindwa kutumia vema udhaifu wa safu ya ulinzi ya wapinzani wao

Timu ya KVZ na Jamhuri zimetoshana nguvu kipindi cha kwanza kwenye mechi yao ya makundi kwenye mashindano ya mapinduzi yanayoendelea kwenye uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Jamhuri ilikuwa na nafasi nzuri ya kuongoza dakika 45 za kwanza lakini ikashindwa kutumia vema udhaifu wa safu ya ulinzi ya wapinzani wao
Kama washambuliaji wa Jamhuri wangekuwa makini dakika ya 44 wangeweza kuandika bao baada ya kipa wa KVZ, Yakoub Bakari Juma kuupanchi mpira wa faulo na kurudi uwanjani,  lakini wachezaji wa Jamhuri walikosa maelewanoa na mpira kuokolewa na mabeki.
Mchezo wake wa Kwanza KVZ ilipoteza mechi yake kwa Yanga baada ya kufungwa mabao 1-0 kwenye dimba la Amaan.

Wao Jamhuri walipata sare kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Azam FC mechi iliyomalizika kwa matokeo ya  sare 1-1.