KMKM yaanza vibaya nyumbani

Saturday August 10 2019

By MOSI ABDALLA, UNGUJA

MAAFANDE wa KMKMya visiwani hapa imeanza vibaya kwenye michuano ya Ligio ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani  dhidi ya Club Desportivo De Agosto kutoka Angola.
Mchezo huo ambao umefanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja  ulijaa mashabiki lukuki kutoka pande mbali mbali za kisiwa cha Unguja  na hivyo Kmkm iliwaangushi mashabiki hao kutokana na kipogo hicho.
Licha ya KMKM kucheza soka zuri la ushindani lakini walijikuta wanafungwa mabao hayo katika kipindi cha pili cha mchezo huo kupitia Manuel David Pfonso dakika 71 na bao la pili likifungwa na mchezaji Lionel Yombi katika dakika 89.
Akizungumza na Mwanaspoti mchambuzi wa soka Zanzibar, Ibrahim Makeresa alisema mfumo ambao wameutumia KMKM ni mgumu kushinda kutokana na kusimamisha mchezaji mmoja mbele.
Alisema mfumo huo ambao waliutumia ulikuwa unatoa nafasi kwa wapinzani wao kucheza na hivyo kupelekea kushambuliwa sana katika lango lao na hivyo kuwapa matokeo wapinzani wao.
Kocha wa KMKM, Ame Msimu amesema katika mchezo huo hawezi kuwalaumu wachezaji wake hasa kwa wameonesha jitihada katika kipindi chote.

Advertisement