KMC yaichapa Coastal mkono, yaishusha Simba

Muktasari:

Katika mchezo huo mabao ya KMC yalifungwa na Charles Ilanfya, Ally Msengi, Emmanuel Mvuyekure, Cliff Buyoya na Elius Maguli, huku Ayoub Lyanga akifunga mabao mawili ya kufutia machozi kwa Coastal Union.

Dar es Salaam. KMC imeishusha Simba hadi nafasi ya nne baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao 5-2 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya KMC kupanda nafasi tatu ikiwa na pointi 34, moja zaidi ya Simba na Mbao zenye pointi 33, huku Yanga ikiongoza Ligi Kuu na pointi 53 na Azam ipo nafasi ya pili ikiwa imekusanya pointi 41.

Katika mchezo huo mabao ya KMC yalifungwa na Charles Ilanfya, Ally Msengi, Emmanuel Mvuyekure, Cliff Buyoya na Elius Maguli, huku Ayoub Lyanga akifunga mabao mawili ya kufutia machozi kwa Coastal Union.

Mshambuliaji Ilanfya alifunga bao la kwanza dakika ya tisa akiwatoka mabeki wa Coastal Union kabla ya kupiga shuti lililomshinda kipa Hussen Shariff.

Msengi alifunga bao la pili kwa kichwa katika dakika 21 akiunganisha mpira uliopigwa na Mvuyekure.

Baada ya kufungwa bao mbili Coastal hawakuonyesha kukatishwa tamaa walipambana, lakini safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Haji Ugando ilikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza hadi mapumziko matokeo 2-0.

Kipindi cha pili Coastal Union ilipata bao lililofungwa na Lyanga kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha upya KMC na kufanikiwa kupata mabao tatu Mvuyekure katika dakika

Lyanga alifunga bao la pili kwa Coastal, lakini kukosa umakini kwa safu ya ulinzi ya mabingwa hao kulitoa mwanya kwa KMC kupata mabao mawili ya haraka katika dakika za mwishoni yaliyofungwa na Boyoya na Maguli aliyehitimisha kalamu hiyo.