KMC yaichakaza Mbao Kirumba

Wednesday May 22 2019

 

By Saddam Sadick

Mwanza. KMC imejiweka katika nafasi katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Mbao FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo Mbao ilionekana kucheza chini ya kiwango na kujikuta wakiwaruhusu wapinzani wao kutakataka kwa ushindi huo na kuendelea kuning'inia nafasi ya nne kwa alama 52.

Bao la kwanza Mbao walijifunga dakika ya pili kupitia kwa Beki wake Babilasi Chitembe wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Aron Lulambo.

KMC walizidi kuliandama zaidi lango la Mbao na dakika ya 38, George Sangija alituma shuti kali nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa Bruno Thomas akikosa la kufanya.

Bao hilo lilionekana kuwakera sana benchi la ufundi la Mbao na kuamua kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Metacha Mnata.

Kipindi cha pili kilionekana kuwa na ushindani kwa Mbao kujaribu kushambulia na kutengeneza nafasi kadhaa, lakini Kipa wa KMC, Jonathan Nahimana kufanya kazi nzuri ya kudhibiti hatari zote.

Advertisement

Advertisement