KIJIWE CHA ANTI K: Hii kwa wakubwa tu!

Muktasari:

Wanaume mnapowakuta wenza wenu wamevaa shanga za rangi nyekundu zote  (hii kwa wanawari wanaojua maana na wenye aibu kusema kuwa mambo yameharibika) ujue hayupo vizuri kujifaragua na wewe hivyo muache hadi atakapokupa ishara nyingine.

Habari wanakwetu. Kama ambavyo wengi wenu mmeomba tuendelee na mada ya kudadavua kuhusu shanga hususani maana ya rangi zake.

Narudia tena shanga ni muhimu kwa mwanamke hasa anapokuwa faragha na mwenza wake.

Shanga hutumika kusisimuana mnapokuwa faragha na hasa mwenza wako anapokuwa anajua kuzitumia vizuri, kama unamvalia wako hazina idadi vaa kulingana na anavyopenda hata kama 10 ilimradi mnafurahia wakati wenu. Usisahau nilikuambia kuwa ni vema ukazivaa muda maalumu kwa kazi maalumu, kuzivaa kisha ukaenda matembezini ni hatari kwa sababu zinaweza kukatika ikawa balaa.

Achana na cheni ni usasa zaidi na faragha haitambui shahada, stashahada wala PhD inahitaji umahiri wako vaa shanga uzungumze kwa kutumia rangi na mwenza wako.

Inawezekana wengi wanavaa kwa ajili ya urembo na kujivalia rangi hovyo hovyo yaani kuchanganya kijani, njano bluu, leo ngoja tukumbushane maana ya rangi za shanga ili wakati mwingine tukikutana na wataalamu wa haya mambo waliofundishwa na bibi zao tusitumie nguvu nyingi kujieleza badala yake kiuno kiwasilishe ujumbe huku kikiburudisha.
Sitokwenda ndani sana (Nitaharibu vibarua vya watu hii ni kazi ya manyakanga jamani) nitawapa kwa uchache tu maana ya rangi za shanga. Nitataja rangi tatu ambazo kwa bahati mbaya wanakwetu wengi mnazivaa kwa pamoja na kuzipotezea maana.
Lakini pia rangi hizo ndiyo zinavaliwa sana.
Wanaume mnapowakuta wenza wenu wamevaa shanga za rangi nyekundu zote  (hii kwa wanawari wanaojua maana na wenye aibu kusema kuwa mambo yameharibika) ujue hayupo vizuri kujifaragua na wewe hivyo muache hadi atakapokupa ishara nyingine.
Najua mmenielewa namaanisha nini, hivyo kwa mwenza mstaarabu akiona hivyo atakufanyia vibweka lakini vya kistaarabu ili asikuchoshe pasi na sababu.
Kuhangaika kulainishana na mwanamke aliyevaa shanga nyekundu zote ni sawa na kuwasha moto usiokuwa na matumizi nao kwa sababu mwisho wa siku hutakuwa na cha kumfanya maana mambo si shwari.

(Kicheko kidogo......)

Mume wa mwenzangu siku ukimkuta mwenza wako amevaa shanga zote rangi nyeupe, nasisitiza zote achana na wanaochanganya rangi, ujue yupo tayari kwa sarakasi.
Hapo unaweza kujifaragua naye utakavyo kwa sababu amekutangazia hali ya amani.
Kizuri zaidi hadi amekuvalia rangi hiyo ujue yupo tayari kwa mtanange, ukijizubaisha unajipunja, hivyo ukikutana na hali hiyo changamkia fursa na uitumie vya kutosha kumkata mwenza wako kiu.
Shughuli ipo hapa wanaume wengi husahau jukumu la kuwasafisha wenza wao, hivyo ukimkuta amevaa zote rangi nyeusi usije kufikiri mwenza wako ameamua kuwa mshirikina, ujue anakukumbusha jukumu hilo muhimu.
Mume wa mwenzangu namaanisha ukimkuta mwenza wako amevaa shanga nyeusi zote ujue anataka umfanyie usafi kabla ya kuzungumza naye kwa herufi kubwa.
Tafadhali usiniangushe kwa kuanza kushangaa shangaa fanya usafi uzungumze kwenye eneo safi.
Niwatakie faragha njema na wenza wenu.