Juve ya Sarri itakavyokuwa!

Muktasari:

Golini atakuwa kipa Wojciech Szczesny, huku safu yake ya mabeki wanne, katikati watakuwa Leonardo Bonucci na Daniele Rugani, wakati kulia atakuwa Elseid Hysaj na kushoto atakuwa Emerson.

TURIN, ITALIA.MAURIZIO Sarri anatua Juventus na tayari imeripotiwa ameshaweka wazi taswira ya kikosi chake kitakavyokuwa kwa msimu ujao.
Sarri ameachana na Chelsea yenye maskani yake huko Stamford Bridge na kutua Juventus baada kununua mkataba wake kwa Pauni 7 milioni na hivyo anakwenda kumbadili Max Allegri huko Turin.
Mpango wa Juventus kwa  sasa ni kumnasa kiungo Paul Pogba na Jorginho, ambaye bila ya shaka atapenda kuandamana na kocha wake huyo alimtoa Napoli kwenda naye Chelsea na sasa anamtaka Juventus. Straika Gonzalo Higuain atarudi kwenye timu yake ya zamani huku timu hiyo ikimtaka pia Emerson. Kama dili zao za wachezaji wanaowataka zitakamilika, basi chama la Juventus litakuwa hivi msimu ujao.
Golini atakuwa kipa Wojciech Szczesny, huku safu yake ya mabeki wanne, katikati watakuwa Leonardo Bonucci na Daniele Rugani, wakati kulia atakuwa Elseid Hysaj na kushoto atakuwa Emerson. Kwenye kiungo kutakuwa na vichwa vitatu, Ramsey akicheza upande wa kushoto, Pogba kulia na katikati ni Jorginho. Pale kwenye fowadi kutakuwa na Ronaldo, Mauro Icardi atakayenaswa kutoka Inter Milan na Higuain.
Hivi ndivyo kikosi cha Juventus kinavyotazamwa kitakavyokuwa kwenye ligi ya msimu ujao huko katika Serie A na Ligi ya Mabingwa Ulaya.