Juuko, Niyonzima wapewa masharti Simba

Wachezaji hao hawajaanza mazoezi ya pamoja na wenzao na wanatarajiwa rasmi kesho

 

BY Waandishi Wetu

IN SUMMARY

  • Wachezaji hao ambao wako jijini Dar es Salaam, walikaa kikao 'kizito' na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' na kufanya makubaliano hayo.

Advertisement

Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba, Juuko Murshid raia wa Uganda na Mnyarwanda Haruna

Niyonzima, wamerudishwa kwenye timu lakini kwa makubaliano maalumu.

Wachezaji hao ambao wako jijini Dar es Salaam, walikaa kikao 'kizito' na Kaimu Rais

wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' na kufanya makubaliano hayo.

Wachezaji hao ambao hawakuwa pamoja na timu kwa kipindi kirefu kutokana na madai ya

utovu wa nidhamu. Sehemu ya masharti yao ni kwenda sawa na matakwa ya klabu.

Wachezaji hao hawajaanza mazoezi ya pamoja na wenzao na wanatarajiwa rasmi kesho

Alhamisi ambapo watafanya pamoja na kikosi cha pili ambacho kitabaki jijini Dar es

Salaam na kocha msaidizi, Mrundi Masoud Djuma.

Baadhi ya wachezaji ambao ni 20, pamoja na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu,

Patrick Aussems isipokuwa Djuma, wataondoka kesho kwa usafiri wa ndege kwenda

Mtwara.

 

 

 

More From Mwanaspoti
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept