Julio asisitiza nidhamu Serengeti Boys

Muktasari:

  • Kingine alichosisitiza, wachezaji wanatakiwa wajengewe kujua ukubwa wa majukumu waliyopewa katika AFCON ya mwaka huu itakayokuwa inashuhudiwa na Watanzania.


KOCHA wa zamani wa Serengeti Boys, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametoa mtazamo wake kuelekea michuano ya AFCON inayofanyika mwaka huu Tanzania wakiwa wenyeji, wachezaji wajengwe kujua faida ya mpira na kupewa motisha ya kujenga akili zao kuwa tayari kwa kazi.

Julio alifichua mbinu alizokuwa anazitumia akiwa kocha wa kikosi hicho alizozitaja alikuwa anawekeza nguvu katika kujenga akili za wachezaji kuikubali kazi ya soka kwa umakini mkubwa na alikuwa anawaaminisha wanategemewa na nchi.

“Kikosi cha sasa hivi sio kibaya, kama alivyosema kocha wao, Oscar Mirambo hawakuandaliwa kwenye misingi ya Akademi lakini haiondoi maana halisi ya ubora walionao.

Kingine alichosisitiza, wachezaji wanatakiwa wajengewe kujua ukubwa wa majukumu waliyopewa katika AFCON ya mwaka huu itakayokuwa inashuhudiwa na Watanzania.