Joh Makini na Mimi Mars hakuna chochote!

Wednesday January 10 2018

 

By Frank Ngobile

RAPA anayetamba na ngoma ya Mipaka, Joh Makini amepangua tetesi zilizosambaa katika mitandao mbalimbali zikimuhusisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mdogo wa Vanessa Mdee, Mimi Mars.

Joh Makini amesema anashangaa taarifa hizo na kufafanua hakuna ukweli wowote kwa sababu Mimi Mars kwake ni sawa na mdogo wake.

“A Big No, Mimi Mars ni kama mdogo wangu, kwanza sisi ni kama familia moja hiyo haiwezi kutokea kabisa,”anasema.

Joh Makini ni mmoja wa wasanii wachache ambao ishu za mahusiano yake yamekuwa ya siri sana hivyo uwepo wa tetesi hizo umewashtua baadhi ya mashabiki wake.