Jinamizi la kesi ya ubakaji lamuandama Ronaldo

Muktasari:

  • Ronaldo alikumbwa na kashfa ya ubakaji mwaka jana wakati alipohama kutoka Real Madrid kwenda Juventus uhamisho uliovunja rekodi Italia msimu huu

London, England. Wakili wa Kathryn Mayorga, mwanamke aliyedai kubakwa na nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo mwaka 2009, atasafiri kwenda London kwa lengo la kukutana na mchumba wa zamani wa Mreno huyo Jasmine Lennard.

Kwa mujibu wa gazeti la USA Today, Leslie Mark Stovall ambaye ni wakili wa Mayorga, atafanya mahojiano na Lennard pamoja na wakili wake, kwa lengo la kupata taarifa zaidi zitakazowasaidi katika kufungua kesi ya mteja wake dhidi ya Ronaldo.

Lennard ni mtangazaji wa TV na mwanamitindo wa England, alitoa taarifa jinsi alivyonyanyaswa kingono na Ronaldo.

Mrembo huyo alituma tumia mara kadhaa Tweets zake kuandika madai wa hayo, ikiwemo lile tishio la Ronaldo kuwa atamteka na kuukata ukata mwili wake nakuweka kwente begi na kuutupa mtoni kama atakuwa na mahusiano na mtu mwingine. Lennard pia amedai kuwa anazo sauti za vitisho hivyo.

Pamoja na kutuma taarifa hizo katika Twitter, Lennard pia alitweeted kuwa yupo tayari kumsaidia katika kesi ya  Mayorga.

Gazeti la USA Today limethibisha kuwa kampuni ya uwakili ya Stovall imefanya mazungumzo ya simu na Lennard na watakwenda London kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Ronaldo kupitia wakili wake wamekataa madai ya Mayorga kuwa alimbaka mwaka 2009, pia wamekataa madai yote yaliyotolewa na Lennard. Ronaldo amesema hata huyo Lennard hamjui.